Wednesday, January 16, 2019

HONGERA MHE RAIS MAGUFULI, PIGA KAZI BABA DUNIA INAONA UNACHOKIFANYA KWA WATANZANIA.


Na Mwandishi wako: Archandramu Mbungu.

Mwaka 2019 umeanza kwa kasi kubwa na ya ajabu sana kwa utawala wa Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuangalia jinsi serikali hii ya awamu ya tano inavyozidi kufanya kazi kubwa na ya kizalendo kama ilivyowaahidi watanzania kipindi cha kampeni. Mwaka huu umeanza kwa matukio makubwa matatu ya kimataifa na ya ndani ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanadhihirisha adhima na nia ya Mhe Rais Magufuli kuwatumikia wanyonge

Ndani ya wiki mbili tu tangu mwaka 2019 uanze, Mhe Rais Magufuli amezidi kuchukua tuzo mbalimbali za kimataifa huku pia nchi yetu chini yake mwenyewe Mhe Rais ikiingia makubaliano ya faida ya uwekezaji kati yake na kampuni ya Airtel.

Twende pamoja kuyaona haya machache katika mengi yanayozidi kuja kwa mwaka 2019.........

HONGERA RAIS MAGUFULI

1. TUZO YA JARIDA NA MTANDAO WA AFRICA54 KWA MHE RAIS MAGUFULI.

Mapema mwanzoni mwa mwaka huu, jarida na mtandao wa Africa54 ulimtaja Mhe Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mzalendo namba moja wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli kushika nafasi ya pili kati ya marais watano bora waliofanya kazi kubwa kwa taifa lao kwa mwaka 2018.

Mtandao huo wa Africa54 katika ripoti yao walisema Rais Magufuli hafanani na Rais yeyote yule barani Afrika aliepo madarakani hasa kwa mda mfupi tu wa utawala wake wa miaka mitatu tu kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko Rais yeyote yule barani Afrika hasa ufanisi wake katika kazi, msimamo na ujasiri wake usioyumbishwa na uongozi wa matukio makubwa ndio umemfanya Rais wetu kuwa miongoni mwa marais watano waliofanya makubwa kwa nchi zao.

Mtandao huo wa Africa54 ambao hutoa ripoti zake kwa kuwauliza wasomaji wake mbalimbali kote duniani, baada ya kukusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wasomaji wake mbalimbali kote duniani ulisema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018 kwa kutoa elimu bure, kuanza kujenga reli ya kisasa ya STANDARD GAUGE RAILWAY( SGR), kufufua shirika la ndege (ATCL)  na kununua ndege kubwa na za kisasa saba (7) na kupiga vita rushwa na ufisadi huku nafasi ya kwanza ikienda kwa rais wa Botswana Tserese Khama La Khama ambae hata hivyo ameshastaafu tangu mwezi aprili mwaka jana.  (SOURCE: AFRICA54 WEBSITE NA MITANDAO YA KIJAMII KAMA YOUTUBE.


2. TUZO NYINGINE YA GAZETI LA AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE (ALM) LA UINGEREZA KWA MHE RAIS MAGUFULI.

Ndani ya wiki hii Mhe rais pia amepata tuzo nyingine kutoka kwa gazeti la African leadership Magazine (ALM) la nchini Uingereza ambapo tuzo hiyo imemtaja Mhe rais Magufuli kama kiongozi bora wa mwaka 2018 kwa upande wa uongozi bora wa siasa na maendeleo huku nafasi ya pili ikienda kwa rais wa Afrika Kusini Ramaphorisa.

Tuzo hii ya heshima ya jamii ya kimataifa kwa kutambua mchango wa rais wetu katika kuleta maendeleo nchini mwake inadhihirisha sio tu watanzania wanaoona juhudi na maendeleo haya yanayotolewa na Mhe Rais Magufuli lakini pia jamii za kimataifa zinaona juhudi hizi na tuzo hii itatolewa tarehe 22 januari mwaka huu mjini Sandton nchini Afrika ya Kusini.

NB: HONGERA RAIS MAGUFULI DUNIA INAONA NA KUHESHIMU UNACHOKIFANYA

3. Makubaliano ya mkataba wa Tanzania na kampuni ya Airtel.

Mwaka 2019, huu ni ushindi mkubwa sana na mwingine kwa Mhe Rais Magufuli na watanzania wote kwa ujumla kwa taifa letu kwa kugeuza uwekezaji wa kampuni ya airtel kuwa uwekezaji wenye tija na manufaa kwa nchi yetu. Nimesikiliza kwa makini sana hotuba ya Mhe Rais majuzi akitia saini makubaliano hayo na kampuni hii ya airtel na nikaona jinsi Mhe Rais alivozungumza kwa uzalendo mkubwa na masikitiko yake kwa suala hili la kampuni ya airtel.

Mhe Rais anasema ndani ya miaka tisa (9) mfululizo ya uwekezaji wa kampuni hii ya airtel nchini, Tanzania ilikuwa haipati chochote (Nchi yetu ilikuwa inapata sifuri kwenye uwekezaji huu wa airtel) kwa maana nchi yetu ilikuwa haifaidiki na chochote na airtel.

Lakini kwa sababu ya serikali hii ya awamu ya tano chini yake mwenyewe Mhe Rais Magufuli ilikataa hiyo na kuamua kuanza majadiliano yaliyochukua miezi nane (8) ili kurekebisha mkataba huo ili sasa nchi yetu ifaidike na mkataba huo na ndipo makubaliano haya yakafikiwa.

Kwa sababu ya Rais Magufuli sasa serikali ya Tanzania imepanda hisa za umiliki wa kampuni ya airtel kutoka 40% hadi 49% huku airtel ikitoa kiasi cha Tsh.Bilioni moja (1) kila mwaka kwa mda wa miaka mitano ya mkataba na serikali yetu ikipata gawio la Tsh. Bilioni kumi (10 ) kwa mwaka......

Kampuni hii ya airtel pia kupitia kwa mwenyekiti wake imetoa ahadi ya kutoa dola za kimarekani Milioni moja (1) sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 2.4 ambazo Mhe rais amezipeleka fedha hizo kwenye miradi mbalimbali nchini kama ya shule, hospitali n.k. huku sehemu ya fedha hizo zikienda kwenye ujenzi wa hospitali ya Uhuru jijini Dodoma.

Hakika ni mwanzo mzuri sana wa mafanikio kwa mwaka 2019 kuelekea ndoto za Rais na taifa letu kuelekea ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 hasa kwa jitihada hizi za kuhakikisha uwekezaji unaofanywa nchini uwe wa WIN by WIN wa kunufaisha pande zote mbili za biashara.

Huu ni ushindi mkubwa sana kwa watanzania wote wa nchi hii kwa namna Mhe Rais anavohakikisha ya kwamba watanzania wote wananufaika na rasilimali na uwekezaji hapa nchini.

 Simu namba 0658245554. 

Monday, November 26, 2018

Breaking news: Ajali mbaya yatokea Mkoa wa Mara leo Tarehe 26/11/2018

Kwa Wana-Mara wote ,imetokea ajali mbaya sana ya kugongana Hiace mbili moja ikienda Musoma nyingine ikitoka Musoma kwenda Tarime maeneo ya Gachuma.Tazama ndg zetu walivyoteketea kwa moto. ZAIDI TAZAMA PICHA HAPO CHINI....




Tuesday, October 2, 2018

BREAKING NEWS: Matokeo ya darasa la saba yafutwa


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.

Miongoni mwa shule zilizokumbana na kadhia hiyo ya kufutwa kwa matokeo hayo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopoHalmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji, Shule za Msingi za halmashauri ya Chemba ambao viongozi wake walitajwa kuhusika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo. Amesema Charles Msonde.

Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.

Monday, September 3, 2018

UPUNGU WA KINGA MWILINI NDIYO CHANZO KIKUU CHA MARADHI MENGI NYEMELEZI (CD4)


Kwa ufupi mpendwa  neno Ukimwi ni kifupisho cha kiingereza AIDS, ni ugonjwa unaotokana na virus ambavyo uitwa VVU ni virus vya ukimwi,kwa kiingereza tunasema HIV (human immunodeficiency virus) na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi nyemelezi
Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo kwa walio wengi na hatimae watu utengwa
Ukimwi umekuwa na madhara makubwa katika jamii na kuhusu ukimwi kama vile unaweza kuambukizwa kwa kugusana nae bila ngono,ugonjwa huu pia unasababisha madhara ya kiuchumi

UPUNGUFU maana yake (ukimwi) unaharibu uwezo wa kupambana na ugonjwa,si ukimwi moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa

1.Kinga inahusu mfumo wa kingamwili ambazo ni uwezo wa mwili kujitetea dhidi ya ugonjwa
2.Mwili usio na kinga ya kutosha unapatwa na matatizo mbali mbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote

Aids maana yake ni nini.?
AIDS-Acquired immunology deficiency syndrome
*ACQUIRED-maana yake mtu awezi kuwa na hali hii kiasili ameipata
*IMMUNE- Hii inataja ya kwamba tatizo linahusu Immune system yani mfumo wa kingamwili
*Deficiency-Inamaanisha ya kwamba kuna kasoro
*SYNDROME-Ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya ili hali kingamwili haufanyi kazi tena,mgonjwa ana athiriwa na magonjwa mbali mbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote

MFUMO WA KINGAMWILI NA VVU

Kila MTU huwa na mfumo Wa kingamwili ndani yake,seli za ulinzi zinazunguka mwili na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu,kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (Lukosaiti) ambayo ni muimu sana

Ukimwi unasababishwa na VVU,kama virus vyote,vvu vinaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa,virus haviwezi kuzaa peke yake vinahitaji seli pindi vinapoweza kuingia ndani ya seli na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake

Kwa kawaida virus vinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika,lakini VVU vina tabia mbili za pekee ambazo zinavifanya mwili kuwa katika hatari
*VVU uwa vinafahulu mara nyingi kuepukana na seli za ulinzi mwilini
*Vinaingia hasa hasa katika seli nyeupe za damu
IMEANDALIWA NA: Archandramu Mbungu
Ni: MNASIHI NA SAIKOLOJISTI
     MWALIMU NA TABIBU KUTUMIA TIBALISHE.
Kwa ushauri, maoni, au tatizo lolote. nitafute kwa namba hii 0766245554
     

Sunday, September 2, 2018

Ajali mbaya imetokea arusha monduli leo

ZAIDI TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA.



ASANTE KWA KUSHIRIKI. MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

Thursday, August 30, 2018

DALILI SABA(7) ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana, ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa utafiti uliofanyika hivi karibuni, mwanaume mmoja kati ya wanaume watatu, wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, mara nyingi upungufu wa nguvu za kiume husababisha mambo mengi.
Kubwa zaidi ni ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini, hilo ni jambo ambalo linaweza kufanyiwa tiba endapo mtu atawahi na linaweza likapona kabisa na likaondoka.Mara nyingi dalili kuu zinazowesha kuashiria mtu anaupungufu wa nguvu za kiume ni kama ifuatavyo:
(1). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSIMAMISHA DHAKARI BARABARA
Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anayekabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara. Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.
(2).KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.
(3).KUTOKUWA NA UWEZO WA KURUDIA TENDO LA NDOA ZAIDI YA MARA MOJA Mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.
(4). UGONJWA WA KISUKARI AU SHINIKIZO LA DAMU(PRESHA)
Watu wenye matatizo haya huwa pia wanapata tatizo hili
(5). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUTOSIMAMISHA KABISA
Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.
(6). UUME KUSINYAA NA KURUDI NDANI
uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.
(7). MSONGO WA MAWAZO
Mtu mwenye msongo wa mawazo au kwa lugha ya kigeni(Stress) muda wote, mambo hayendi kama unavyotaka, akili inakuwa imejazwa na mawazo mengi basi moja kwa moja hata ule mfumo unaoratibu hisia zako kwenye suala la mapenzi linakuwa halipo.

WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WALIMU WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI KUONESHA UMAHIRI KATIKA KUFUNDISHA STADI ZA KKK

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka walimu walioshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo wa kumudu Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuonesha umahiri unaotakiwa katika kufundisha Stadi hizo ili kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili pindi watakaporejea katika vituo vyao vya kazi.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo hayo ambapo amesema pamoja na mambo mengine ana imani kuwa kupitia mafunzo hayo walimu wa darasa la kwanza na la pili wameongeza mbinu ambazo watazitumia kuwafundishia wanafunzi waweze kumudu stadi hizo kwani ndio msingi bora wa kumudu masomo yanayofundishwa kwenye darasa la tatu hadi darasa la saba.

“Nyumba imara hujengwa na msingi imara hivyo mafunzo haya ni muhimu sana kwenu walimu mnaofundisha Darasa la kwanza na la pili ili muweze kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema masomo katika ngazi za Elimu zinazofuata” Alisisitiza Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na walimu (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK. Amewataka walimu hao kutumia mbinu walizopata, upendo na hamasa kuwafundisha watoto ili wapate ujuzi na maarifa yatakayoleta tija katika Taifa

Waziri Ndalichako alisema lengo la Serikali ni kuendelea kuwapatia walimu wengi mafunzo ya ufundishaji wa Stadi za KKK pamoja na mbinu zingine za ufundishaji.

“Mtakumbuka Agosti 18, 2018 nilizindua matumizi ya Vikaragosi katika kufundisha Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu kwa Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili jijini Dar es Salaam, hizi zote ni juhudi za Serikali kuhakiksha ufundishaji unaimarika na wanafunzi wanaelewa” Aliongeza Waziri Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea Kitabu cha Picha kama zawadi kutoka kwa walimu walioshiriki mafunzo ya kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mjini Morogoro.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amewataka Walimu wote nchini kuunga mkono juhudi za serikali za kuunda bodi ya utaalamu wa walimu kwa kuwa ina lengo la kuutambua ualimu kama taaluma na utaalamu ikiwa ni pamoja na kulinda hadhi ya mwalimu.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kumudu Stadi za KKK yanatolewa kwa walimu 1600 wa mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Mwanza na Tanga ambayo shule zake zina mkondo zaidi ya mmoja. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akigawa cheti kwa mmoja wa walimu walioshiriki mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mkoani Morogoro.