Afisa Elimu Msingi wilaya ya Mbinga vijijini Ndg.Samweli Komba ametoa ufafanuzi waraka wa elimu bure katika kikao cha tathimini ya elimu kilichofanyika wilaya ya Mbinga vijijini tarafa ya Mbuji tarehe 23/ 05/ 2018. Kikao hicho kiliwahusisha afisa elimu taaluma na mkaguzi wa elimu wilaya, maafisa elimu kata, wakuu wa shule, watendaji wa vijijji, wenyeviti wa vijiji na wadau mbalimbali wa elimu. Katika kikao hicho Afisa Elimu Ndg Samweli Komba aliwasomea waraka wa elimu na kuwafafanulia maana harisi wa waraka huo na kuondoa dhana potofu iliyojikita kwa jamii kuwa haitakiwi kuchangia mchango wowote shuleni, bali michango lazima iwe ili kuleta maendeleo shuleni. Afisa huyo aliwaeleza kuwa michango lazima ipate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wilaya.
Afisa elimu Ndug, Samweli Komba akiwa amesimama kutolea maelezo ya kina juu ya waraka wa elimu.
Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa wanamsikiliza Afisa Elimu
Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa wanamsikiliza Afisa Elimu
Afisa Elimu akiwa mbele ya wadau wa elimu akitolea ufafanuzi wa waraka wa elimu bure
No comments:
Post a Comment