Na Mwandishi wako: Archandramu Mbungu.
Mwaka 2019 umeanza kwa kasi kubwa na ya ajabu sana kwa utawala wa Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuangalia jinsi serikali hii ya awamu ya tano inavyozidi kufanya kazi kubwa na ya kizalendo kama ilivyowaahidi watanzania kipindi cha kampeni. Mwaka huu umeanza kwa matukio makubwa matatu ya kimataifa na ya ndani ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanadhihirisha adhima na nia ya Mhe Rais Magufuli kuwatumikia wanyonge
Ndani ya wiki mbili tu tangu mwaka 2019 uanze, Mhe Rais Magufuli amezidi kuchukua tuzo mbalimbali za kimataifa huku pia nchi yetu chini yake mwenyewe Mhe Rais ikiingia makubaliano ya faida ya uwekezaji kati yake na kampuni ya Airtel.
Twende pamoja kuyaona haya machache katika mengi yanayozidi kuja kwa mwaka 2019.........
HONGERA RAIS MAGUFULI
1. TUZO YA JARIDA NA MTANDAO WA AFRICA54 KWA MHE RAIS MAGUFULI.
Mapema mwanzoni mwa mwaka huu, jarida na mtandao wa Africa54 ulimtaja Mhe Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mzalendo namba moja wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli kushika nafasi ya pili kati ya marais watano bora waliofanya kazi kubwa kwa taifa lao kwa mwaka 2018.
Mtandao huo wa Africa54 katika ripoti yao walisema Rais Magufuli hafanani na Rais yeyote yule barani Afrika aliepo madarakani hasa kwa mda mfupi tu wa utawala wake wa miaka mitatu tu kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko Rais yeyote yule barani Afrika hasa ufanisi wake katika kazi, msimamo na ujasiri wake usioyumbishwa na uongozi wa matukio makubwa ndio umemfanya Rais wetu kuwa miongoni mwa marais watano waliofanya makubwa kwa nchi zao.
Mtandao huo wa Africa54 ambao hutoa ripoti zake kwa kuwauliza wasomaji wake mbalimbali kote duniani, baada ya kukusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wasomaji wake mbalimbali kote duniani ulisema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018 kwa kutoa elimu bure, kuanza kujenga reli ya kisasa ya STANDARD GAUGE RAILWAY( SGR), kufufua shirika la ndege (ATCL) na kununua ndege kubwa na za kisasa saba (7) na kupiga vita rushwa na ufisadi huku nafasi ya kwanza ikienda kwa rais wa Botswana Tserese Khama La Khama ambae hata hivyo ameshastaafu tangu mwezi aprili mwaka jana. (SOURCE: AFRICA54 WEBSITE NA MITANDAO YA KIJAMII KAMA YOUTUBE.
2. TUZO NYINGINE YA GAZETI LA AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE (ALM) LA UINGEREZA KWA MHE RAIS MAGUFULI.
Ndani ya wiki hii Mhe rais pia amepata tuzo nyingine kutoka kwa gazeti la African leadership Magazine (ALM) la nchini Uingereza ambapo tuzo hiyo imemtaja Mhe rais Magufuli kama kiongozi bora wa mwaka 2018 kwa upande wa uongozi bora wa siasa na maendeleo huku nafasi ya pili ikienda kwa rais wa Afrika Kusini Ramaphorisa.
Tuzo hii ya heshima ya jamii ya kimataifa kwa kutambua mchango wa rais wetu katika kuleta maendeleo nchini mwake inadhihirisha sio tu watanzania wanaoona juhudi na maendeleo haya yanayotolewa na Mhe Rais Magufuli lakini pia jamii za kimataifa zinaona juhudi hizi na tuzo hii itatolewa tarehe 22 januari mwaka huu mjini Sandton nchini Afrika ya Kusini.
NB: HONGERA RAIS MAGUFULI DUNIA INAONA NA KUHESHIMU UNACHOKIFANYA
3. Makubaliano ya mkataba wa Tanzania na kampuni ya Airtel.
Mwaka 2019, huu ni ushindi mkubwa sana na mwingine kwa Mhe Rais Magufuli na watanzania wote kwa ujumla kwa taifa letu kwa kugeuza uwekezaji wa kampuni ya airtel kuwa uwekezaji wenye tija na manufaa kwa nchi yetu. Nimesikiliza kwa makini sana hotuba ya Mhe Rais majuzi akitia saini makubaliano hayo na kampuni hii ya airtel na nikaona jinsi Mhe Rais alivozungumza kwa uzalendo mkubwa na masikitiko yake kwa suala hili la kampuni ya airtel.
Mhe Rais anasema ndani ya miaka tisa (9) mfululizo ya uwekezaji wa kampuni hii ya airtel nchini, Tanzania ilikuwa haipati chochote (Nchi yetu ilikuwa inapata sifuri kwenye uwekezaji huu wa airtel) kwa maana nchi yetu ilikuwa haifaidiki na chochote na airtel.
Lakini kwa sababu ya serikali hii ya awamu ya tano chini yake mwenyewe Mhe Rais Magufuli ilikataa hiyo na kuamua kuanza majadiliano yaliyochukua miezi nane (8) ili kurekebisha mkataba huo ili sasa nchi yetu ifaidike na mkataba huo na ndipo makubaliano haya yakafikiwa.
Kwa sababu ya Rais Magufuli sasa serikali ya Tanzania imepanda hisa za umiliki wa kampuni ya airtel kutoka 40% hadi 49% huku airtel ikitoa kiasi cha Tsh.Bilioni moja (1) kila mwaka kwa mda wa miaka mitano ya mkataba na serikali yetu ikipata gawio la Tsh. Bilioni kumi (10 ) kwa mwaka......
Kampuni hii ya airtel pia kupitia kwa mwenyekiti wake imetoa ahadi ya kutoa dola za kimarekani Milioni moja (1) sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 2.4 ambazo Mhe rais amezipeleka fedha hizo kwenye miradi mbalimbali nchini kama ya shule, hospitali n.k. huku sehemu ya fedha hizo zikienda kwenye ujenzi wa hospitali ya Uhuru jijini Dodoma.
Hakika ni mwanzo mzuri sana wa mafanikio kwa mwaka 2019 kuelekea ndoto za Rais na taifa letu kuelekea ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 hasa kwa jitihada hizi za kuhakikisha uwekezaji unaofanywa nchini uwe wa WIN by WIN wa kunufaisha pande zote mbili za biashara.
Huu ni ushindi mkubwa sana kwa watanzania wote wa nchi hii kwa namna Mhe Rais anavohakikisha ya kwamba watanzania wote wananufaika na rasilimali na uwekezaji hapa nchini.
Simu namba 0658245554.
No comments:
Post a Comment