Monday, November 26, 2018
Breaking news: Ajali mbaya yatokea Mkoa wa Mara leo Tarehe 26/11/2018
Tuesday, October 2, 2018
BREAKING NEWS: Matokeo ya darasa la saba yafutwa
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.
Miongoni mwa shule zilizokumbana na kadhia hiyo ya kufutwa kwa matokeo hayo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopoHalmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji, Shule za Msingi za halmashauri ya Chemba ambao viongozi wake walitajwa kuhusika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo. Amesema Charles Msonde.
Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.
Monday, September 3, 2018
UPUNGU WA KINGA MWILINI NDIYO CHANZO KIKUU CHA MARADHI MENGI NYEMELEZI (CD4)
Kwa ufupi mpendwa neno Ukimwi ni kifupisho cha kiingereza AIDS, ni ugonjwa unaotokana na virus ambavyo uitwa VVU ni virus vya ukimwi,kwa kiingereza tunasema HIV (human immunodeficiency virus) na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi nyemelezi
Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo kwa walio wengi na hatimae watu utengwa
Ukimwi umekuwa na madhara makubwa katika jamii na kuhusu ukimwi kama vile unaweza kuambukizwa kwa kugusana nae bila ngono,ugonjwa huu pia unasababisha madhara ya kiuchumi
UPUNGUFU maana yake (ukimwi) unaharibu uwezo wa kupambana na ugonjwa,si ukimwi moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa
1.Kinga inahusu mfumo wa kingamwili ambazo ni uwezo wa mwili kujitetea dhidi ya ugonjwa
2.Mwili usio na kinga ya kutosha unapatwa na matatizo mbali mbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote
Aids maana yake ni nini.?
AIDS-Acquired immunology deficiency syndrome
*ACQUIRED-maana yake mtu awezi kuwa na hali hii kiasili ameipata
*IMMUNE- Hii inataja ya kwamba tatizo linahusu Immune system yani mfumo wa kingamwili
*Deficiency-Inamaanisha ya kwamba kuna kasoro
*SYNDROME-Ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya ili hali kingamwili haufanyi kazi tena,mgonjwa ana athiriwa na magonjwa mbali mbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote
MFUMO WA KINGAMWILI NA VVU
Kila MTU huwa na mfumo Wa kingamwili ndani yake,seli za ulinzi zinazunguka mwili na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu,kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (Lukosaiti) ambayo ni muimu sana
Ukimwi unasababishwa na VVU,kama virus vyote,vvu vinaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa,virus haviwezi kuzaa peke yake vinahitaji seli pindi vinapoweza kuingia ndani ya seli na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake
Kwa kawaida virus vinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika,lakini VVU vina tabia mbili za pekee ambazo zinavifanya mwili kuwa katika hatari
*VVU uwa vinafahulu mara nyingi kuepukana na seli za ulinzi mwilini
*Vinaingia hasa hasa katika seli nyeupe za damu
IMEANDALIWA NA: Archandramu Mbungu
Ni: MNASIHI NA SAIKOLOJISTI
MWALIMU NA TABIBU KUTUMIA TIBALISHE.
Kwa ushauri, maoni, au tatizo lolote. nitafute kwa namba hii 0766245554
Sunday, September 2, 2018
Thursday, August 30, 2018
DALILI SABA(7) ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana, ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa utafiti uliofanyika hivi karibuni, mwanaume mmoja kati ya wanaume watatu, wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, mara nyingi upungufu wa nguvu za kiume husababisha mambo mengi.
Kubwa zaidi ni ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini, hilo ni jambo ambalo linaweza kufanyiwa tiba endapo mtu atawahi na linaweza likapona kabisa na likaondoka.Mara nyingi dalili kuu zinazowesha kuashiria mtu anaupungufu wa nguvu za kiume ni kama ifuatavyo:
(1). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSIMAMISHA DHAKARI BARABARA
Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anayekabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara. Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.
(2).KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.
(3).KUTOKUWA NA UWEZO WA KURUDIA TENDO LA NDOA ZAIDI YA MARA MOJA Mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.
(4). UGONJWA WA KISUKARI AU SHINIKIZO LA DAMU(PRESHA)
Watu wenye matatizo haya huwa pia wanapata tatizo hili
(5). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUTOSIMAMISHA KABISA
Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.
(6). UUME KUSINYAA NA KURUDI NDANI
uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.
(7). MSONGO WA MAWAZO
Mtu mwenye msongo wa mawazo au kwa lugha ya kigeni(Stress) muda wote, mambo hayendi kama unavyotaka, akili inakuwa imejazwa na mawazo mengi basi moja kwa moja hata ule mfumo unaoratibu hisia zako kwenye suala la mapenzi linakuwa halipo.
WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WALIMU WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI KUONESHA UMAHIRI KATIKA KUFUNDISHA STADI ZA KKK
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka walimu walioshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo wa kumudu Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuonesha umahiri unaotakiwa katika kufundisha Stadi hizo ili kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili pindi watakaporejea katika vituo vyao vya kazi.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo hayo ambapo amesema pamoja na mambo mengine ana imani kuwa kupitia mafunzo hayo walimu wa darasa la kwanza na la pili wameongeza mbinu ambazo watazitumia kuwafundishia wanafunzi waweze kumudu stadi hizo kwani ndio msingi bora wa kumudu masomo yanayofundishwa kwenye darasa la tatu hadi darasa la saba.
“Nyumba imara hujengwa na msingi imara hivyo mafunzo haya ni muhimu sana kwenu walimu mnaofundisha Darasa la kwanza na la pili ili muweze kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema masomo katika ngazi za Elimu zinazofuata” Alisisitiza Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na walimu (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK. Amewataka walimu hao kutumia mbinu walizopata, upendo na hamasa kuwafundisha watoto ili wapate ujuzi na maarifa yatakayoleta tija katika Taifa
Waziri Ndalichako alisema lengo la Serikali ni kuendelea kuwapatia walimu wengi mafunzo ya ufundishaji wa Stadi za KKK pamoja na mbinu zingine za ufundishaji.
“Mtakumbuka Agosti 18, 2018 nilizindua matumizi ya Vikaragosi katika kufundisha Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu kwa Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili jijini Dar es Salaam, hizi zote ni juhudi za Serikali kuhakiksha ufundishaji unaimarika na wanafunzi wanaelewa” Aliongeza Waziri Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea Kitabu cha Picha kama zawadi kutoka kwa walimu walioshiriki mafunzo ya kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mjini Morogoro.
Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amewataka Walimu wote nchini kuunga mkono juhudi za serikali za kuunda bodi ya utaalamu wa walimu kwa kuwa ina lengo la kuutambua ualimu kama taaluma na utaalamu ikiwa ni pamoja na kulinda hadhi ya mwalimu.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kumudu Stadi za KKK yanatolewa kwa walimu 1600 wa mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Mwanza na Tanga ambayo shule zake zina mkondo zaidi ya mmoja.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akigawa cheti kwa mmoja wa walimu walioshiriki mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mkoani Morogoro.
Monday, August 20, 2018
MATATIZO YA HEDHI NA TIBA YAKE KWA WANAWAKE
Na Archandramu Mbungu.
KILA mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika.
DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.
MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.
Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.
JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.
Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.
Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.
TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.
UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.
Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.
PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)
Wednesday, August 8, 2018
BREAKINGNEWS Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018
BREAKINGNEWS Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018alipokuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zimethibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyo wa sanaa ambaye amejizolea umaarufu kila pembe ya Nchi yetu.
Taarifa zaidi ya wapi ulipo msiba na taratibu zote za mazishi zitakujia baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.
R.I.P KING MAJUTO
Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zimethibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyo wa sanaa ambaye amejizolea umaarufu kila pembe ya Nchi yetu.
Taarifa zaidi ya wapi ulipo msiba na taratibu zote za mazishi zitakujia baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.
R.I.P KING MAJUTO
Tuesday, August 7, 2018
Mhe. Jokate :Nidhamu,Bidii,Ushirikiano Vitaijenga Kisarawe
Ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia, Mkuu wa Wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amekutana na watumishi wa Wilaya ya Kisarawe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Kutaniko hilo limefanyika siku ya jumatatu ambapo lengo kubwa likiwa ni kutambulishana ,kufahamiana na kuweka mikakati jinsi ya kuwahudumia wananchi katika kuleta maendeleo yao na Wilaya kwa ujumla
Awali wakati anamkaribisha Mkuu wa Wilaya azungumze na watumishi ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba aliwatambulisha watumishi hao mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa kutambulisha watumishi hao kwa kila idara na vitengo na kueleza kwa kifupi matarajio ya watumishi kwa ujio wa mkuu a wilaya mpya
Akihutbia kutaniko hilo Mkuu wa Wilaya alianza kwa kujitambulisha na kuelezea matumaini makubwa ya ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika kuwahudumia wananchi wa kisarawe na kuwaletea maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye utekelezaji wa mipango ya serikalia inaytekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Aidha Mkuu wa Wilaya huyo amebainisha mambo makuu matatu ambayo kwa pamoja yakifuatwa yataleta tija kubwa kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi
‘’ lengo kuu la kukuatana hapa ni kufahamiana na kuwekana sawa na tutakuwa watumishi wa mfano bora na wa kuigwa .Mkusayiko huu unaashiria vitu vingi,unaashiria mshikamano.ili tusonge mbele tunahitaji kuwa na nidhamu ya kazi, bidii na ushirikiano’’ amesema mheshimiwa Jokate Mwegelo
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Patric Allute amesema wanamkaribisha na watumishi wamemsikiliza na watatekeleza maaagizo yote ili kuweza kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Monday, August 6, 2018
SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA WAKATI
Na:ARCHANDRAMU MBUNGU.
AMENORRHEA NI NINI??
hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi/kupitiliza siku za hedhi
~kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani
~kuna aina mbili za tatizo hili (amenorrhea)
(1)PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke/msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo Hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile KUOTA NYWELE SEHEMU ZA SIRI, KUOTA MATITI, NK ila bado hapati siku zake
(2)SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida Lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa
~NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio Sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa
~VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika Makundi makuu matatu ambayo ni vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo katika tezi ya pituitar, mfumo wa Uzazi na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke visababishi hivyo ni ÷
👉matatizo katika hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha ÷uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar, ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi,
👉uzito mdogo kuliko Kawaida
👉pituitar kushindwa kufanya Kaz vzur baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
👉kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)
(proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo Hali ya kuwa proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi
👉kuwa na msongo wa mawazo ni hatari
👉kuziba kwa utando unaozunguka uke (HYMEN) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)
👉 Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri yani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari
👉ugonjwa wa kurithi wa GALACTOSEMIA unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya GALACTOSE katika damu
👉baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
👉MENO PAUSE ~hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42_55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi hufanya haziwezi kufanya Kazi sawasawa
DALILI ZA TATIZO HILI
👉Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za ANDROGEN
👉kuongezeka uzito kupita kiasi
👉matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
👉mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
👉 uke kuwa mkavu
👉kutokwa jasho sana wakati wa usiku
👉mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries
👉kutokupata hedhi katika mpangilio
MATIBABU
NA JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji pale patapobidi
NOTE :Ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiepusha na tatizo hili
👉ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
👉TUMIA MAZIWA YA SOY /JUICE YA WATERMELON/MAJI YA MSHUBIRI
👉FANYA MASAJI KWENYE TUMBO LA CHINI KWA KUTUMIA MAJI YA UVUGUVUGU (UKIWA KTK BREED) HII ITASAIDIA KUONGEZA DAMU NYINGI KUTOKA
👉KULA CHAKULA KISICHOTOKANA NA DAMU (VEGETARIAN DIET) CHENYE PROTIN NYINGI MFANO, NAZI, MAHARAGE, KOROSHO NA KARANGA
Hakikisha unazingatia haya ili kuepukana na madhara ya huu ugonjwa ambayo ni makubwa sana
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU
👉Mwanamke kuchelewa kuingia menopause hali huu ni mbaya kwani husababisha SARATAN YA MATITI kwa kias kikubwa
👉mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu
👉husababisha matatzo ya kutopata usingizi
👉matiti husinyaa na kupata hedhi Bila mpangilio,
Saturday, August 4, 2018
MKUU WA JESHI LA POLISI WILAYA YA MBINGA NDUGU RAMIA MGANGA AMETOA MAELEKEZO YA USALAMA BARABARANI KWA MAAFISA ELIMU KATA LEO TAREHE 04/08/2018
Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Mbinga ndugu Ramia Mganga ametoa maelekezo muhimu ya matumizi mazuri ya barabara na usalama barabarani.
Mkuu huyo ametoa maelekezo hayo leo katika viwanja vya polisi vilivyopo kituo kikuu cha polisi Mbinga akiwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wa wilaya ambapo kila mmoja alitoa elimu ya usalama barabarani kwa maafisa elimu hao na kutoa msisitizo juu ya umuhimu wa matumizi mazuri ya barabara.
Aidha mkuu huyo aliwaeleza maafisa elimu hao kuwa kila Afisa elimu kata anatakiwa awe na leseni ili iwasaidie kuendesha vyombo vya moto barabarani.Kama Afisa hana leseni ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi Mbinga chini ya mkuu wa kitengo cha usalama barabarani itawasaidia katika zoezi la kupata leseni hizo, kikubwa wao waandae pesa za kushughulikia zoezi la upatikanaji wa leseni.
Pia aliwaeleza umuhimu wa kuvaa elementi kwani inazuia majeraha ya kichwani na hata kupasuka kichwa kunakopelekea vifo vingi, wawe waangalifu wakiwa barabarani kwa kufuata alama za barabara kwa umakini ili kuepusha ajali zisizo na msingi.
Kwa upande wa Mkuu wa usalama barabrani wilaya ya Mbinga aliwasisitiza maafisa hao kupata mafunzo ya udereva ili wapate vyeti vinavyotambulika serikalini, wazingatie alama za barabarani,waepuke kubeba abilia,mizigo ya biashara na kutumia pikipiki za serikali nje ya muda wa kazi.
Pia aliwaelimisha umuhimu wa stika za usalama barabarani, bima na kuvikagua vyombo vyao vya usafiri mara kwa mara ili viwe katika hali ya usalama daima.
ZAIDI TAZAMA PICHA HAPO CHINI.⇩
Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Mbinga ndugu Ramia Mganga kushoto na kulia ni mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Mbinga.
Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.
Mwenyekiti wa maafisa elimu kata akiuliza swali
Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.
Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.
Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.
Tuesday, July 31, 2018
MKUU WA WILAYA YA MBINGA MH. COSMAS NSHENYE AMEONGOZA ZOEZI LA KUWAKABIDHI MAAFISA ELIMU KATA PIKIPIKI ZA SERIKALI KATIKA OFISI ZA MKURUGENZI MTENDAJI LEO TAREHE 30/07/2018
Kabla ya zoezi hilo kuanza Mh. Samweli Komba mbaye ni afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga alisoma taarifa fupi mbele ya uongozi wa wilaya na umati uliokusanyika eneo hilo kushuhudia zoezi hilo la ugawaji wa pikipiki.
Mh.Samweli Komba alisema serikali imetoa pikipiki hizo ili kuwasaidia maafisa elimu hao katika shughuli zao za kikazi.Pia alisisitiza kuwa pikipiki hizo zitumike kwa shughuli za kikazi tu na zisaidie kutokomeza tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma kuandika na kuhesabu.
Mh. Samweli Komba aliwasihi maafisa elimu kata hao wasizitumie pikipiki hizo kwa maswala ya biashara mfano bodaboda, kubebea mazao, na kukodisha. Alisema atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Aidha Mh. COSMAS NSHENYE ambaye ni Mkuu wa wilaya ya mbinga aliwasihi pia maafisa elimu hao kuwa wasije chezea vyombo vya serikali kwa maslahi yao binafsi. Aliwaeleza maafisa hao wahakikishe kabla ya kuanza kuzitumia wawe na leseni.Alisema pikipiki hizo zikatumiwe kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. Kisha alifungua zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa kuzindua kuendesha pikipiki moja.
ZAIDI TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPO CHINI.
Mkuu wa wilaya na maafisa elimu kata wakikagua pikipiki kabla ya zoezi la kuwakabidhi.
Afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga vijijini Mh. Samweli Komba akiwaelekeza maafisa juu ya matumizi ya pikipiki hizo.
Maafisa elimu kata wakiwa makini kusikiliza maelekezo
Maafisa elimu kata wakiwa makini kusikiliza maelekezo
Maafisa elimu kata wakiwa makini kusikiliza maelekezo
Mkuu wa wilaya ya Mbinga DC akiwaelekeza maafisa maelekezo ya utumiaji wa pikipiki
Afisa wa ngazi ya juu wa Tusome Pamoja akishuhudia zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa maafisa lililoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbinga.
Maafisa wakiwa katika furaha ya kupewa pikipiki
Maafisa elimu kata wakijadiliana namna ya kukitunza chombo hicho
Maafisa elimu kata wakisubiri kukabidhiwa pikipiki
Afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga akisoma taarifa fupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya.
Hizi ni baadhi ya pikipiki za maafisa elimu kata
Maafisa wakiwa makini kusikiliza maelekezo
Wakuu wa idala ngazi ya wilaya ya Mbinga DC wakiwa sehemu ya tukio akishuhudia
Afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga akiwasisitiza maafisa elimu kata matumizi mazuri mbele Mkuu wa wilaya ya Mbinga
Mkuu wa wilaya ya Mbinga akiwa anajiandaa kuzindua pikipiki, aliyeshikilia ni Afisa elimu msingi taaluma Mh.Chusi.
Subscribe to:
Posts (Atom)