Thursday, August 30, 2018

DALILI SABA(7) ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana, ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa utafiti uliofanyika hivi karibuni, mwanaume mmoja kati ya wanaume watatu, wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, mara nyingi upungufu wa nguvu za kiume husababisha mambo mengi.
Kubwa zaidi ni ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini, hilo ni jambo ambalo linaweza kufanyiwa tiba endapo mtu atawahi na linaweza likapona kabisa na likaondoka.Mara nyingi dalili kuu zinazowesha kuashiria mtu anaupungufu wa nguvu za kiume ni kama ifuatavyo:
(1). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSIMAMISHA DHAKARI BARABARA
Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anayekabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara. Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.
(2).KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.
(3).KUTOKUWA NA UWEZO WA KURUDIA TENDO LA NDOA ZAIDI YA MARA MOJA Mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.
(4). UGONJWA WA KISUKARI AU SHINIKIZO LA DAMU(PRESHA)
Watu wenye matatizo haya huwa pia wanapata tatizo hili
(5). KUTOKUWA NA UWEZO WA KUTOSIMAMISHA KABISA
Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.
(6). UUME KUSINYAA NA KURUDI NDANI
uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.
(7). MSONGO WA MAWAZO
Mtu mwenye msongo wa mawazo au kwa lugha ya kigeni(Stress) muda wote, mambo hayendi kama unavyotaka, akili inakuwa imejazwa na mawazo mengi basi moja kwa moja hata ule mfumo unaoratibu hisia zako kwenye suala la mapenzi linakuwa halipo.

WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA WALIMU WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI KUONESHA UMAHIRI KATIKA KUFUNDISHA STADI ZA KKK

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka walimu walioshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo wa kumudu Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuonesha umahiri unaotakiwa katika kufundisha Stadi hizo ili kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili pindi watakaporejea katika vituo vyao vya kazi.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo hayo ambapo amesema pamoja na mambo mengine ana imani kuwa kupitia mafunzo hayo walimu wa darasa la kwanza na la pili wameongeza mbinu ambazo watazitumia kuwafundishia wanafunzi waweze kumudu stadi hizo kwani ndio msingi bora wa kumudu masomo yanayofundishwa kwenye darasa la tatu hadi darasa la saba.

“Nyumba imara hujengwa na msingi imara hivyo mafunzo haya ni muhimu sana kwenu walimu mnaofundisha Darasa la kwanza na la pili ili muweze kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema masomo katika ngazi za Elimu zinazofuata” Alisisitiza Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na walimu (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK. Amewataka walimu hao kutumia mbinu walizopata, upendo na hamasa kuwafundisha watoto ili wapate ujuzi na maarifa yatakayoleta tija katika Taifa

Waziri Ndalichako alisema lengo la Serikali ni kuendelea kuwapatia walimu wengi mafunzo ya ufundishaji wa Stadi za KKK pamoja na mbinu zingine za ufundishaji.

“Mtakumbuka Agosti 18, 2018 nilizindua matumizi ya Vikaragosi katika kufundisha Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu kwa Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili jijini Dar es Salaam, hizi zote ni juhudi za Serikali kuhakiksha ufundishaji unaimarika na wanafunzi wanaelewa” Aliongeza Waziri Ndalichako
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea Kitabu cha Picha kama zawadi kutoka kwa walimu walioshiriki mafunzo ya kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mjini Morogoro.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako amewataka Walimu wote nchini kuunga mkono juhudi za serikali za kuunda bodi ya utaalamu wa walimu kwa kuwa ina lengo la kuutambua ualimu kama taaluma na utaalamu ikiwa ni pamoja na kulinda hadhi ya mwalimu.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kumudu Stadi za KKK yanatolewa kwa walimu 1600 wa mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Kagera, Mwanza na Tanga ambayo shule zake zina mkondo zaidi ya mmoja. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akigawa cheti kwa mmoja wa walimu walioshiriki mafunzo ya uimarishaji wa Stadi za KKK wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Morogoro, Mkoani Morogoro.

Monday, August 20, 2018

MATATIZO YA HEDHI NA TIBA YAKE KWA WANAWAKE


Na Archandramu Mbungu.
KILA mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika.

DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.

TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

Wednesday, August 8, 2018

BREAKINGNEWS Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018

BREAKINGNEWS Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018alipokuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zimethibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyo wa sanaa ambaye amejizolea umaarufu kila pembe ya Nchi yetu.

Taarifa zaidi ya wapi ulipo msiba na taratibu zote za mazishi zitakujia baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.
R.I.P KING MAJUTO






Tuesday, August 7, 2018

Mhe. Jokate :Nidhamu,Bidii,Ushirikiano Vitaijenga Kisarawe

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia,  Mkuu wa Wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amekutana na watumishi wa Wilaya ya Kisarawe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Kutaniko hilo limefanyika siku ya jumatatu ambapo lengo kubwa likiwa ni  kutambulishana ,kufahamiana na kuweka mikakati jinsi ya kuwahudumia wananchi katika kuleta maendeleo yao na  Wilaya kwa ujumla

Awali  wakati anamkaribisha  Mkuu wa Wilaya azungumze na watumishi ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba aliwatambulisha watumishi hao mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa kutambulisha watumishi hao kwa kila idara na vitengo na kueleza kwa kifupi matarajio ya watumishi kwa ujio wa mkuu a wilaya mpya

Akihutbia kutaniko hilo Mkuu wa Wilaya alianza kwa kujitambulisha na kuelezea matumaini makubwa ya ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika kuwahudumia wananchi wa kisarawe na kuwaletea maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye utekelezaji wa mipango ya serikalia inaytekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Aidha Mkuu wa Wilaya huyo  amebainisha  mambo makuu matatu ambayo kwa pamoja yakifuatwa yataleta tija kubwa kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi

‘’  lengo kuu la kukuatana hapa ni kufahamiana na kuwekana sawa na tutakuwa watumishi wa mfano bora na wa kuigwa .Mkusayiko huu unaashiria vitu vingi,unaashiria mshikamano.ili tusonge mbele tunahitaji kuwa na nidhamu ya kazi, bidii na ushirikiano’’ amesema mheshimiwa Jokate Mwegelo

Kaimu  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Patric Allute amesema wanamkaribisha na watumishi wamemsikiliza na watatekeleza maaagizo yote ili kuweza kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Monday, August 6, 2018

SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA WAKATI


Na:ARCHANDRAMU MBUNGU.

AMENORRHEA NI NINI??
hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi/kupitiliza siku za hedhi
~kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani
~kuna aina mbili za tatizo hili (amenorrhea)
(1)PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke/msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo Hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile KUOTA NYWELE SEHEMU ZA SIRI, KUOTA MATITI, NK ila bado hapati siku zake
(2)SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida Lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa
~NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio Sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa
~VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika Makundi makuu matatu ambayo ni vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo katika tezi ya pituitar, mfumo wa Uzazi na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke visababishi hivyo ni ÷
👉matatizo katika hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha ÷uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar, ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi,
👉uzito mdogo kuliko Kawaida
👉pituitar kushindwa kufanya Kaz vzur baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
👉kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)
(proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo Hali ya kuwa proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi
👉kuwa na msongo wa mawazo ni hatari
👉kuziba kwa utando unaozunguka uke (HYMEN) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)
👉 Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri yani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari
👉ugonjwa wa kurithi wa GALACTOSEMIA unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya GALACTOSE katika damu
👉baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
👉MENO PAUSE ~hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42_55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi hufanya haziwezi kufanya Kazi sawasawa
DALILI ZA TATIZO HILI
👉Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za ANDROGEN
👉kuongezeka uzito kupita kiasi
👉matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
👉mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
👉 uke kuwa mkavu
👉kutokwa jasho sana wakati  wa usiku
👉mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries
👉kutokupata hedhi katika mpangilio
MATIBABU
NA JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji pale patapobidi
NOTE :Ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiepusha na tatizo hili
👉ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
👉TUMIA MAZIWA YA SOY /JUICE YA WATERMELON/MAJI YA MSHUBIRI
👉FANYA MASAJI KWENYE TUMBO LA CHINI KWA KUTUMIA MAJI YA UVUGUVUGU (UKIWA KTK BREED) HII ITASAIDIA KUONGEZA DAMU NYINGI KUTOKA
👉KULA CHAKULA  KISICHOTOKANA NA DAMU (VEGETARIAN DIET) CHENYE PROTIN NYINGI MFANO, NAZI, MAHARAGE, KOROSHO NA KARANGA
Hakikisha unazingatia haya ili kuepukana na madhara ya huu ugonjwa ambayo ni makubwa sana
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU
👉Mwanamke kuchelewa kuingia menopause hali huu ni mbaya kwani husababisha SARATAN YA MATITI kwa kias kikubwa
👉mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu
👉husababisha matatzo ya kutopata usingizi
👉matiti husinyaa na kupata hedhi Bila mpangilio,


Saturday, August 4, 2018

MKUU WA JESHI LA POLISI WILAYA YA MBINGA NDUGU RAMIA MGANGA AMETOA MAELEKEZO YA USALAMA BARABARANI KWA MAAFISA ELIMU KATA LEO TAREHE 04/08/2018

Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Mbinga ndugu Ramia Mganga ametoa maelekezo muhimu ya matumizi mazuri ya barabara na usalama barabarani.

Mkuu huyo ametoa maelekezo hayo leo katika viwanja vya polisi vilivyopo kituo kikuu cha polisi Mbinga akiwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wa wilaya ambapo kila mmoja alitoa elimu ya usalama barabarani kwa maafisa elimu hao na kutoa msisitizo juu ya umuhimu wa matumizi mazuri ya barabara.

Aidha mkuu huyo aliwaeleza maafisa elimu hao kuwa kila Afisa elimu kata anatakiwa awe na leseni ili iwasaidie kuendesha vyombo vya moto barabarani.Kama Afisa hana leseni ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi Mbinga chini ya mkuu wa kitengo cha usalama barabarani itawasaidia katika zoezi la kupata leseni hizo, kikubwa wao waandae pesa za kushughulikia zoezi la upatikanaji wa leseni.

Pia aliwaeleza umuhimu wa kuvaa elementi kwani inazuia majeraha ya kichwani na hata kupasuka kichwa kunakopelekea vifo vingi, wawe waangalifu wakiwa barabarani kwa kufuata alama za barabara kwa umakini ili kuepusha ajali zisizo na msingi.

Kwa upande wa Mkuu wa usalama barabrani wilaya ya Mbinga aliwasisitiza maafisa hao kupata mafunzo ya udereva ili wapate vyeti vinavyotambulika serikalini, wazingatie alama za barabarani,waepuke kubeba abilia,mizigo ya biashara na kutumia pikipiki za serikali nje ya muda wa kazi.
Pia aliwaelimisha umuhimu wa stika za usalama barabarani, bima na kuvikagua vyombo vyao vya usafiri mara kwa mara ili viwe katika hali ya usalama daima.
ZAIDI TAZAMA PICHA HAPO CHINI.⇩ 
Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Mbinga ndugu Ramia Mganga kushoto na kulia ni mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Mbinga.

Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.

Mwenyekiti wa maafisa elimu kata akiuliza swali

Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.

Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.

 Hawa ni baadhi ya maafisa elimu kata wakisikiliza kwa makini maelekezo.