Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Mikoa, Wizara na Wilaya.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho huo ili kujaza nafasi zilizo wazi kufuatia baadhi ya viongozi kustaafu, kuteuliwa katika nafasi nyingine na wengine kuachwa.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo;
1. Bw. ALLY SALUM HAPI (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya AMINA MASENZA ambaye amestaafu.
2. Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU ambaye amestaafu.
3. Bw. ALBERT CHALAMILA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Bw. AMOS GABRIEL MAKALA ambaye amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL MUHUGA amestaafu.
4. Brigedia Jenerali NICODEMAS ELIAS MWANGELA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi ya Luteni Mstaafu CHIKU GALLAWA ambaye amestaafu.
Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa kama ifuatavyo:
1. Bw. KESSY MADUKA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MADENGE
2. Bw. ABOUBAKAR MUSSA KUNENGE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Bibi THERESIA MMBANDO.
3. Bw. DAVID KAFULILA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
4. Bw. DENIS BANDISA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya SELESTINE GESIMBA
5. Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Bibi. WAMOJA DICKOLAGWA.
6. Bw. ABDALLAH MOHAMED MALELA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
7. Bw. RASHID KASSIM MCHATA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Bw. CHARLES PALLANGYO.
8. Bw. MISSAILE MUSSA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
9. Bi. CAROLINE ALBERT MTHAPULA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MARA.
10. Dkt. JILLY ELIBARIKI MALEKO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya ALFRED LUANDA.
11. Bw. CHRISTOPHER DEREK KADIO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Mstaafu CLODWING MTWEVE.
12. Bw. ERIC SHITINDI ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Anachukua nafasi ya BW. JACKSON SAITABAU.
13. Prof. RIZIKI SALAS SHEMDOE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Bw. HASSAN BENDEYEKO.
Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya kazi.
1. Bibi REHEMA MADENGE aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DODOMA, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.
2. Bibi THERESIA MMBANDO aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DAR ES SALAAM amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kwa baadhi ya Wizara kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. JOSEPH BUCHWESHAIJA kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Anachukua nafasi ya Prof. ELISANTE Ole GABRIEL.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. ANDREW WILSON MASSAWE kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. ELISANTE Ole GABRIEL kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo).
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)
5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. EDWIN PAUL MHEDE kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na wengine kuhamishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JERRY CORNEL MURO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. FRANK JAMES MWAISUMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Anachukua nafasi ya Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PATROBAS KATAMBI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi MWANAHAMISI ATHUMAN MUKUNDA kuwa Mkuu wa Wilaya ya BAHI. Anachukua nafasi ya ELIZABETH SIMON KITUNDU.
5. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido kwenda Wilaya ya Kinondoni.
6. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bibi SARA MSAFIRI ALLY aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwenda Wilaya ya Kigamboni. Anachukua nafasi ya Bw. HASHIM SHAIBU MGANDILWA.
7. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. SAID MKUMBA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Anachukua nafasi ya JOSEPHAT PAULO MAGANGA
8. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bw. JOSEPHAT PAULO MAGANGA na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Anachukua nafasi ya HERMAN CLEMENT KAPUFI.
9. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali PATRICK NORBERT SONGEA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Anachukua nafasi ya SHAABAN ATHUMAN NTARAMBE.
10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. RASHID MOHAMED MWAIMU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa. Anachukua nafasi ya Kanali SHABAN ILANGU LISSU
11. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali SIMON M. ANANGE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.
12. Mhe. Rais Magufuli amemteua Luteni Kanali MICHAEL MASALAMA NGAYALINA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe. Anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI.
13. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. LENGAI Ole SABAYA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
14. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. HASHIM SHAIBU MGANDILWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa. Anachukua nafasi ya Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI.
15. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ELIZABETH SIMON KITUNDU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati. Anachukua nafasi ya RAYMOND HIERONIMI MUSHI
16. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang. Anachukua nafasi ya SARA MSAFIRI ALLY.
17. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. MARY-PRISKA WINFRED MAHUNDI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MANASE MADUSA.
18. Mhe. Rais Magufuli amemteua Ndg. NGOLLO MALENYA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga. Anachukua nafasi ya Bw. JACOB JOSEPH KASSOMA.
19. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. MOSES JOSEPH MACHALI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
20. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. SEVERIN MATHIAS LALIKA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.
21. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILIS MESHACK NYIMBO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. Anachukua nafasi ya MARY ONESMO TESHA.
22. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILEMON SENGATI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu. Anachukua nafasi ya HADIJA RASHID NYOMBO.
23. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali LUCAS BONIPHACE MAGEMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe. Anachukua nafasi ya ESTOMIH FRANCIS CHANG’AH.
24. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ZAINAB RASHID MFAUME KAWAWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo. Anachukua nafasi ya Bw. MAJID HEMED MWANGA.
25. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. JOKATE MWEGELO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Anachukua nafasi ya Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM.
26. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. SOPHIA KIZIGO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo. Anachukua nafasi ya Bibi. LUCKINESS ADRIAN AMLIMA.
27. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. JASINTA VENANT MBONEKO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Anachukua nafasi ya JOSEPHINE RABBY MATIRO.
28. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. RAHABU MWAGISA SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
29. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PASACAS MURAGIRI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya ELIAS CHORO JOHN TARIMO.
30. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. KOMANYA ERIC KITWALA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
31. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. KISA KASONGWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.
Tarehe ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa itatangazwa baadaye.
Wakuu wa Wilaya wataapishwa na Wakuu wao wa Mikoa kwa utaratibu utakaopangwa na Mikoa husika.
No comments:
Post a Comment